advertise with us

ADVERTISE HERE

UCHAMBUZI WA AMOSPOTI: KIKOSI PENDEKEZWA CHA SIMBA LEOKikosi cha Simba kitakachoanza leo dhidi ya Yanga Uwanja wa Taifa, kwa mujibu wa  www.amospoti.com na sababu zimetajwa namna hii:-

Kipa: Aish Manula,rekodi zinambeba kuonekana kuwa bora kuliko mlinda mlango namba mbili Beno Kakolanya, leo ana kazi ya kuwa makini kuepuka lawama za bao lile la Mapinduzi Balama.

Beki wa Kulia, Shomary Kapombe, yupo fiti kwa sasa na anazidi kuwabora akiwapoteza wenzake ndani ya kikosi.

Beki wa Kushoto, Mohamed Hussein 'Tshabalala', nahodha huyu Msaidizi yupo fiti na ana spidi akiwa ndani ya Uwanja, mabao mawili mguuni kwa sasa.

Beki wa Kati: Pascal Wawa, kipenzi cha Sven Vandenbroeck ana nafasi ya kuanza leo amecheza kwenye mechi tano mfululizo akikosa moja tu dhidi ya Stand United ilikuwa ya Shirikisho.

Beki wa Kati, Eraso Nyoni, alikosa mechi iliyopita Januari 4, ila kwa sasa ameonekana kurejea kwenye ubora.

Kiungo Mchezeshaji, Clatous Chama, makali yake kwenye mechi ya Azam yalionekana alikuwa akipoa na timu inapoa, mguuni ana asisti saba na mabao mawili.

Mshambuliaji, John Bocco, mtambo wa mabao hasa kwa mfumo wa 4-4-2 yeye anaiweza akiwa kati, mabao matatu kwa sasa na pasi moja ya bao.

Mshambuliaji, Meddie Kagere, mtambo wa mabao ndani ya Simba ana urafiki na nyavu za Yanga, mchezo uliopita alimtungua Shikalo kwa penalti

Winga, Francis Kahata, pasi sita za mabao, mabao manne mguuni nafasi kubwa kwake.

Winga, Luis Misqussone, kipenzi cha mashabiki, ana pasi moja ya bao na mabao matatu mguuni.

Post a Comment

0 Comments