BETI NASI UTAJIRIKE

UCHAMBUZI WA AMOSPOTI: KIKOSI PENDEKEZWA CHA YANGA LEO


Kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kuanza leo dhidi ya Simba, leo Machi 8, Uwanja wa Taifa kwa mujibu wa www.amospoti.com na sababu zake zatajwa:-

Kipa: Farouk Shikalo, uzoefu unambeba alikuwa langoni kwenye dabi ya Januari 4, Uwanja wa Taifa, Simba 2-2 Yanga.

Beki wa Kulia: Juma Abdul inaonyesha amerejea kwenye ubora wake kwa sasa na amekuwa imara.

Beki wa Kushoto: Jafary Mohamed, kipenzi cha Kocha Mkuu, Luc Eymael.

Beki wa Kati, Lamine Moro, uwezo wa mghana huyu unaimarika kila iitwapo leo akiwa uwanjani.

Beki wa Kati: Kelvin Yondani, bado uzoefu wake unambeba licha ya kutokuwa kwenye mechi za hivi karibuni.

Kiungo Mkabaji: Papy Tshishimbi, alikuepo kwenye dabi ya Januari 4, uzoefu unambeba

Kiungo Mchezeshaji: Haruna Niyonzima, uzoefu na kasi yake vinambeba.

Winga: Balama Mapinduzi, mshuti wake bado unaishi, wengi wanatarajia kuona maajabu kwake

Mshambuliaji:- Tariq Seif, Amecheza mechi tatu za hivi karibuni akimuweka benchi, David Molinga mbele ya Coastal Union, Gwambina, Alliance

Mshambuliaji wa Kati: Ditram Nchimbi, mwili wenye nguvu na mishuti mikali, anapewa nafasi ya kuanza akiwa amefunga abao mawili ndani ya Yanga

Winga: Bernard Morrison, kiungo mshambuliaji raia wa Ghana kipenzi cha mashabiki ana nafasi ya kuanza jumla kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uimara wake.

Post a Comment

0 Comments