advertise with us

ADVERTISE HERE

UCHAMBUZI : LIVERPOOL VS ATLETICO MADRID NA PSG VS BORUSSIA DORTMUNDLigi ya mabingwa Ulaya inaendelea leo usiku wa saa tano kwa kuzikutansha timu nne kwenye mechi mbili za mtoano. Liverpool itakuwa mwenyeji wa Atletico madrid mchezo utakaopigwa Anfield wakati PSG itaikaribisha Borrusia Dortmund kwenye mchezo utakaopigwa dimba Le Parc des princes 

Uchambuzi mdogo

Paris Saint Germain Vs Borrusia Dortmund 

Mchezo wa kwanza ulimalizika kwa PSG kupokea kipigo cha mabao 2-1 ikiwa ugenini. Leo wapo nyumbani na watatakiwa kutumia nguvu zote kuhakikisha wanashinda bao 1-0 na kuendelea ,kama watapata sare basi safari yao itaishia hapo . Kocha Tomas Tuchel atatakiwa awatumie Icardi, Neymar  na Kylian Mbappe kama washambuliaji huku akiimalisha safu ya ulinzi na kiungo. Kocha Tuchel atatakiwa kuchezesha mpira wa kasi ili kuharibu mipango ya Dortmund.

Dortmund wao hawana cha kupoteza na wanachokitafuta ni sare ya aina yeyote na wanatakiwa kushinda. Uwepo wa mshambuliaji Haaland ,Sancho na Thiago Hazard kutaongeza nguvu ya Dortmund eneo la ushambuliaji.

NB: Kocha Thomas Tuchell aliwahi kuiongoza Dortmund toka mwaka 2015 mpaka 2017 huku 2018 akitua PSG. Uwepo wake kama mwalimu wa zamani wa Dortmund unaweza kumpa nguvu ya kushinda mchezo huo.

Liverpool Vs Atletico Madrid

Mchezo wa kwanza ulimalizika kwa Liverpool kupigwa bao 1-0 na Atletico Madrid na hawakufanikiwa kupiga shuti lolote lililolenga lango. Leo usiku wanakazi ngumu ya kuhakikisha wanapat ushidi wa mabao 2-0 na kuendelea. Kama mchezo utamalizika kwa mabao 2-1 Liverpool watayaaga mashindano na sare yoyote itawaondoa kwenye michuano. Michezo. 

Atletico anauwezo wa kushinda na kufuzu hatua ya robo Fainali endapo tu atashinda mchezo huo au sare ya aina yeyote. Uwepo wa Diego Costa ,Morata na Correo unaweza kuzaa matunda.

NB: Liverpool huwa hatari sana inapocheza uwanja wa Anfield lakini pia uwepo wa Sadio Mane ,Salah na DFirmino utaimalisha safu ya ushambuliaji.

Mechi hizi zitapigwa saa 5 usiku huu. Tukutane kesho asubuhi pale  Lemutuz tv kuuzungumzia mchezo huo.


Post a Comment

0 Comments