BETI NASI UTAJIRIKE

TSHISHIMBI ATOA SABABU ZA YANGA KUFUNGWA NA KMC


Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa sababu iliyowafanya wakapoteza mbele ya KMC ni kubadilishiwa uwanja uliopangwa kuchezwa awali jambo lililowaathiri kisaikolojia.

Awali mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru Machi 12 na Yanga kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 ulipaswa uchezwe Uwanja wa Taifa.

"Tulikuwa tunajua kwamba tutacheza Uwanja wa Taifa ila tukaambiwa kwamba mchezo utachezwa Uhuru jambo hilo kiasi chake limetufanya saikolojia isiwe sawa, lakini kwa kuwa ni mpira matokeo tumeyakubali na tunawapongeza wapinzani kwa kutumia nafasi moja waliyoipata," amesema.

 Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo imepoteza mechi nne baada ya kucheza mechi 26 kwenye Ligi Kuu Bara.

Post a Comment

0 Comments