TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TREHE 23-03-2020

Baba wa mchezaji wa Real Madrid Luka Jovic, 22, amesema mtoto wake inabidi akubali adhabu yoyote - hata kufungwa- endapo atakutwa na hatia ya kukiuka masharti ya karantini kwa kusafiri kwenda kumtembelea mpenzi wake jijini Belgrade. (Marca)
Barcelona wana nia ya kumsajili beki wa Manchester City na Ufaransa Aymeric Laporte, 25, katika majira ya kiangazi.(Mundo Deportivo - in Spanish)
Klabu za Paris St-Germain, Real Madrid na Manchester City zote zinawania kumsajili beki wa Inter Milan na timu ya taifa ya Slovakia Milan Skriniar, 25. (Calciomercato - in Italian)
Kalidou Koulibaly, 28, yupo tayari kuihama klabu ya Napoli mwishoni mwa msimu, huku Manchester United ikihusishwa na kutaka kumsajili beki huyo wa kati wa Senegal. (Mirror)
Barcelona wapo tayari kumuuza mshambuliaji wao Mfaransa are Antoine Griezmann, 29, kwa dau la Euro milioni 100 - ikiwa ni mwaka mmoja tu toka walipomsajili kwa dau la Euro milioni 120 akitokea klabu ya Atletico Madrid for 120m euros. (Sport)
Liverpool na Arsenal walikuwa wanamfuatilia beki wa klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani Evan Ndicka, 20, kabla ya msimu kusimamishwa. (Sky Sports)
Arsenal wapo katika mazungumzo na madaktari wa klabu nyengine za Ligi ya Premia juu ya uwezekano wa wachezaji wake kuanza mazoezi wiki hii. (Mail)
Mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 32, amevunja masharti ya Karantini nchini Italia na kusafiri mpaka Argentina kwenda kumuuguza mama yake ambaye anaumwa saratani. (Sun)
Barcelona wapo katika mazungumzo na wachezaji wao nyota ili kupunguza mishahara yao kutokana na klabu hiyo kuona kuwa haitaweza kuhimili bajeti ya mishahara inayofikia Euro bilioni 1 kwa kipindi cha msimu kilichobakia. (Marca)
Kiungo wa zamani wa Arsenal na Barcelona Alexander Hleb amedai "hakuna mtu anayejali" kuhusu virusi vya corona nchini mwake Belarus nchi pekee ambayo bado inaendelea na ligi kuu kwa sasa. (Sun)

Post a Comment

0 Comments