Mshambuliaji wa Manchester United na Nigeria Odion Ighalo, 30, ambaye yuko klabu hiyo kwa mkopo kutoka Shanghai Shenhua, anajiandaa kupunguziwa mshahara hadi £6m ili asalie katika ligi ya primia. (Mail)
Klabu hiyo inayochezea Old Trafford pia inapigiwa upatu kusajili kiungo wa kati wa Ajax Donny van de Beek, nayo Real Madrid huenda ikamkosa kiungo wa kimataifa wa Uholanzi wa miaka 23. (Marca - in Spanish)
Juventus inajiandaa kuwasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji wa Portugal Cristiano Ronaldo, 35, mkataba ambao utarefusha uwepo wake katika klabu hiyo ya Italia hadi mwaka 2024. (Tuttosport via Mail)
Mshambuliaji wa England na Tottenham Harry Kane, 26, huenda akasusia uhamisho wa fedha nyingi wa kuenda Manchester United au Manchester City na badala yake kujiunga na Juventus. (Tuttosport via Express)
Manchester City wanatumia muda uliowekwa wa kuahirisha ligi ya Primia kujadili mkataba mpya wa wachezaji Kevin De Bruyne, 28, na Raheem Sterling, 25. (Sun)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anamtaka beki wa West Ham ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £60m Issa Diop, 23, ambaye pia ananyatiwa na Manchester United. (Metro)
Mshambuliaji wa Birmingham City Jude Bellingham anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuamua ahamie wapi kati ya klabu nne zinazomtaka- Manchester United, Chelsea, Bayern Munich and Borussia Dortmund - ambao wako tayari kulipa £30m kumpata Muingereza huyo wa miaka 16. (Sun)
Barcelona, Manchester United na Real Madrid zitamenyana kumpata kiungo wa kati wa Fenerbahce Mturuki Omer Beyaz, 16. (Express)
Kipa wa mkopo wa Sheffield United Dean Henderson, 23, anatarajiwa kurejea katika klabu yake ya Manchester United msimu wa joto licha ya Chelsea kuonesha nia ya kutaka kumnunua. (Star)
Tottenham imekuwa ikimnyatia kiungo wa kati mshambulizi wa Queens Park Rangers Eberechi Eze, 21, huku klabu hiyo ya Loftus Road ikitarajiwa kuitisha £20m kumuachilia kiungo huyo wa chini ya miaka 21. (Sun)
Mashabiki wametoa wito kwa wamiliki wa West Ham, David Sullivan na David Gold kuuza klabu hiyo licha ya ongezeko la kutoridhishwa kwao na utendakazi wake. (Telegraph)
0 Comments