TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATANO TAREHE 18-03-2020

Real Madrid wanapanga mikakati itakayomuwezesha mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 30, kuondoka kwa uhamisho bila malipo. (Marca)
Manchester City wametanga £80m kuwa bei ya kumuuza winga wa Algeria Riyad Mahrez, 29, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuenda Paris St-Germain. (Sun)
Manchester United wanapanga 'mkakati' wa kusaini mkataba na beki wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti, 26 msimu huu. (Talksport)
Beki wa Atletico Madrid na Kieran Trippier, 29, amedokeza kuwa atastaafu katika klabu yake ya zamani Burnley na kwamba atarejea katika ligi ya Primia ikiwa atacheza Turf Moor chini ya Sean Dyche. (Sky Sports)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumuuza kiungo wa kati wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 31, msimu wa joto huku wakiwa na mpango wa kubadili mkataba ake wa mkopo kuwa uhamisho wa kudumu . (Express)

Henrikh MkhitaryanHaki miliki ya picha

West Ham imesema wanaamini wataweza kucheza mechi zao za nyumbani katika uwanja wa London ikiwa msimu huu utaingia majira ya joto, licha ya mashindano ya baseball, riadha na matamasha ya muziki ambayo yanatarajiwa kufanyika katika uwanja huo. (Standard)
Mmiliki wa Chelsea Mrusi Roman Abramovich, 53, ameripotiwa kushuka kwa thamani ya mali yake kwa hadi £2.4bn mwaka huu kutokana na mlipuko wa coronavirus japo thamani yake inakadiriwa kuwa zaidi ya £10bn. (Star)

Jetro WillemsHaki miliki ya picha

Beki Mdachi Jetro Willems, 25, ambaye yuko Newcastle kutoka klabu ya Ujerumani ya Eintracht Frankfurt, hatacheza tena mwaka 2020 baada ya kupata jeraha la goti. (Bild, via Newcastle Chronicle)
Kipa wa Bournemouth Mbosnia Asmir Begovic, 32, ambaye yupo AC Milan kwa mkopo, amesema kuondoka Milana ni sawa na tukio la kuigiza katika filamu wakati huu ambapo Italia inakabiliwa na janga la ugonjwa wa Corona

Post a Comment

0 Comments