TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATANO TAREHE 11-03-2020


Real Madrid huenda ikamtimua kocha wake Zinedine Zidane na kumuajiri aliyekuwa kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino ama aliyekuwa kocha wa Juventus Massimiliano Allegri.(Marca - in Spanish)
Atletico Madrid inasalia na nia kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre lacazette ,28, kutoka Arsenal. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Barcelona imemweka mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 24, kama chaguo la pili nyuma ya mshambuliaji wa Inter Milan na Lautaro Martinez, 22. (Mundo Deportivo - in Spanish)
  • Timo warner
Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, alifanyiwa vipimo vya corona kabla ya mechi ya klabu bingwa kati ya Paris-St Germain dhidi ya Borussia Dortmund - na kuonekana hana maambukizi ya ugonjwa huo. (L'Equipe - in French)
Aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson anajaribu kuisaidia klabu hiyo kumsaini Jude Bellingham kutoka Birmingham baada ya kukutana na wazazi wa kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 16 wakati walipotembelea uwanja wa mazoezi wa Old Trafford siku ya Jumatatu(Star)
Beki wa Monaco na Ufaransa Djibril Sidibe, 27, anasema kwamba anataka mkataba wake katika klabu ya Everton kuwa wa kudumu. (RMC Sport, via Liverpool Echo)

Djibril Sidibe

Liverpool inatumaini kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Jeremy Doku, 17, baada ya uhamisho wa awali wa kinda huyo kugonga mwamba. (Het Nieuwsblad, via Star)
Wakala Mino Raiola anasema kwamba mawakala wengine wakuu wanaunga mkono mipango mingine ya mfumo mbadala wa uhamisho ambao unaweza kuiharibu Fifa vibaya.. (Telegraph - subscription required)
Uefa inafikiria kuahirisha michuano ya Euro 2020 kwa mwaka mmoja kutokana na mlipuko wa virusi vya corona kufuatia maombi yaliowasilishwa na mashirika tofauti ya soka duniani. (Tuttosport - in Italian)

Mino Raiola

Wakala Jorge Alvial aliwasilisha ripoti 40 katika klabu ya Manchester United kuhusu uhamisho wa Alphonso Davies - kabla ya Bayern Munich kumsaini winga huyo wa Canada , 19, kutoka Vancouver Whitecaps. (Sun)
Arsenal inajaribu kuimarisha hatma ya winga wa England Bukayo Saka, 18, huku Man United wakivutiwa na mchezaji huyo. (Express)

Post a Comment

0 Comments