advertise with us

ADVERTISE HERE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMANNE TAREHE 31-03-2020

Liverpool hawana mpango wa kumsajili tena kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 27, ambaye yuko Bayern Munich kwa mkopo kutoka Barcelona. (Mirror)
Manchester United wameelekeza darubini yao kwa kiungo wa kati wa Leicester City na England James Maddison, 23, baada ya nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24, ambaye wamekuwa wakimnyatia kwa
muda mrefu kuhusishwa na kisa cha utata nje ya uwanja. (Daily Star)
Real Madrid wanamfuatilia karibu nyota wa Sao Paulo Igor Gomes, 21, maarufu 'Kaka mpya' huku Barcelona, Sevilla na Ajax pia wakimng'ang'ania mchezaji huyo wa safu ya kati ya Brazili wa chini ya miaka 20. (AS)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 31, amedokeza kuwa ataendelea kucheza katika Ligi Kuu ya soka ya England endapo ataondoka Stamford Bridge, hatua ambayo huenda ikafufua matumaini ya
Arsenal na Tottenham kumsaka. (ESPN Brazil - in Portuguese)
James MaddisonHaki miliki ya pichan
Klabu za Arsenal, Tottenham na West Ham zinamnyatia beki wa Liverpool Dejan Lovren, 30, mkataba wake ukielekea ukingoni Anfield. (Teamtalk)
Beki wa wa mkopo wa Arsenal Dani Ceballos, 23, yuko tayari kuhamia Real Betis tbadala ya kusalia katika uwanja wa Emirates, ikiwa klabu Real Madrid haitaki tena huduma ya nyota huyo wa Uhispania.(Estadio Deportivo via Express)
Real Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal raia wa Gabon Emerick Aubameyang,30, endapo watashindwa kumpata Erling Braut Haaland, 19, kutoka Borussia Dortmund ama mchezaji wa kimataifa wa Senegal Sadio Mane, 27 kutoka Liverpool. (Express)
Mshambuliaji wa Arsenal raia wa Gabon Emerick AubameyangHaki miliki ya pichan
Real pia wanataka kumsajili kiungo wa kati Mbrazili wa miaka 21, Igor Gomes, ambaye bei yake huenda ikawa £45m kutoka Sao Paolo.(AS - in Spanish)
Newcastle United wanapania kuwasajili kwa mkopo wachezaji wa safu ya kati ya Robbie Brady na Jeff Hendrick, walio na miaka 28. Mkataba wa wachezaji hao wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland katika uwanja wa
Turf Moor unamalizika msimu huu wa joto. (Newcastle Chronicle)
Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan ana matumaini ya uhamisho wake wa mkopo kwenda Roma utageuzwa kuwa mkataba wa kudumu msimu huu . Arsenal wanataka £18m kumuachilia kiungo huyo wa miaka 31- raia wa Armenia, lakini klabu hiyo ya Italia inataka kulipa £10m tu. (Mail)

Post a Comment

0 Comments