Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo mwenye miaka 30, amepewa ofa ya kuongezewa mkataba wa miaka miwili na timu yake ya China Shanghai Shenhua huku mshahara ukipanda mpaka paundi 400,000 kwa wiki. (Sky Sports)
Vilabu vya EFL vimeambiwa ligi haitarudi Aprili 30 na tarehe mpya ya kurejea kwa EFL itatangazwa wiki ijayo wakati mapambano dhidi ya kirusi corona yakiendelea.(Mail)
Real Madrid wana nia ya kumsaini Erling Braut Haaland, 19, kutoka Borussia Dortmund msimu wa joto. Mshambuliaji huyo wa Norway kwenye mkataba wake kunakipengere cha kuuzwa kwa pauni 50m. (Standard)
Everton ni moja wapo ya vilabu vinne ambavyo wametoa ofa ya mlinzi wa Mbrazil, Lille, 23, ambaye anagharimu karibu pauni 30m. (Sky Sports)
Arsenal ina hamu ya kusajili kiungo wa Valencia wa Uhispania Carlos Soler, 23. (Sky Sports)
Manchester United wanampango wa kumuongezea mkataba kiungo wake Paul Pogba, 27, Kiungo wa kati wa Uhispania Pedro, 32, ameweka wazi ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu wakati mkataba wake na Blues utakuwa umemalizika. (AS - in Spanish)
Barcelona waitamani saini ya mchezaji wa ghali zaidi wa Tottenham Tanguy Ndombele, 23, ambaye alijiunga na timu hiyo ya kaskazini mwa London kwa pauni 55m kutoka Lyon msimu wa joto uliopita. (Mundo Deportivo via Star)
Tottenham wamefungua mazungumzo ya awali na kiungo wa kati wa Kiingereza Oliver Skipp, 19, juu ya mpango mpya wa muda mrefu. (Football Insider)
Chelsea, Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich wote wamekuwa wakiwinda saini ya kiungo wa kimataifa wa vijana wa Espanyol Nico Melamed, 18, ambaye ana kifungu cha kutolewa cha pauni 7.3m.(Mundo Deportivo via Star)
West Ham, Sporting Lisbon na Anderlecht ni kati ya vilabu vinavyo mtazama kipa wa Liverpool wa Ujerumani, Loris Karius, 26, ambaye yupo kwa mkopo Besiktas na anapatikana kwa pauni milioni 4.5 mwishoni mwa msimu. (Voetbal24 - in Dutch)
West Brom wanataka kumchukua moja kwa moja beki wa kati wa Croatia Filip Kronvinovic ambayo yupo kwa mkopo, ikiwa watarudi ligi kuu. (Mail)
0 Comments