TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO IJUMAA TAREHE 13-03-2020

Arsenal inajiandaa kuwasilisha ombi la kumsajili mchezaji wa Atletico Madrid Thomas Partey. Kiungo huyo wa Ghana, 26, ana kifungu cha pauni milioni 45 ili kuondoka katika klabu hiyo (Telegraph)
Juventus itakabiliana na Arsenal naTottenham kumsajili mshambuliaji huru wa Chelsea Willian, licha ya mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 30 kutaka kusalia jijini London. (Tuttosport via Sport Witness)
Phil Neville anafikiria kujiuzulu kama mkufunzi wa timu ya wanawake ya England baada ya timu hiyo kulazwa mara 12. (Mail)
Mchezaji wa Chelsea Willian
Arsenal inatarajia kwamba mechi zake mbili zitaahirishwa baada ya mkufunzi wa Arsenal kukutwa na virusi vya corona. (Mirror)
Klabu za ligi ya Premia hazitaki kuwaachilia wachezaji wake kwa likizo ya kimataifa mwezi huu kutokana na hofu ya virusi vya corona. (Mail)
Muungano wa shirikisho la soka Ulaya Uefa na ule wa klabu katika eneo hilo utapendekeza michuano ya Euro 2020 kuahirishwa kwa mwaka kutoa fursa kwa mechi za ligi za Europa zilizocheleweshwa kutokana na virusi vya corona kukamilishwa kabla ya mwisho wa msimu huu. (Mirror)
Vitesse Arnhem inatamani kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea na England Conor Gallagher, 20, kwa mkopo kwa msimu ujao. (Sun)
Conor Gallaghe
Everton inatamani kumpata mshambuliaji wa Italia Andrea Belotti, 26, kutoka Torino. (Calciomercato- in Italian)
Shirikisho la soka la EFL nchini England linaunga mkono klabu ya West Brom katika mgogoro wao na Barcelona kuhusu kumsaini mshambuliaji wa England Louie Barry, ambaye amejiunga na Aston Villa. (Express and Star)
Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba yuko tayari kuufanya uhamisho wa mshambuliaji wa Odion Ighalo' kuwa wa kudumu . mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amefunga magoli manne katika mechi nane tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Shanghai Shenhua mwezi Januari. (Manchester Evening News)
Odion Ighalo
Mshambuliaji wa Chelsea anayetarajiwa Hakim Ziyech, 26, angependelea kuishawishi klabu hiyo kumsajili kipa wa Nigeria Andre Onana, 23, kutoka klabu ya Ajax (Mail)

Post a Comment

0 Comments