BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO IJUMAA TAREHE 6-3-2020

Mshambuliaji wa Manchester United Mnigeria Odion Ighalo, 30, ambaye anachezea klabu hiyo kwa mkopo kutoka Shanghai Shenhua inayoshiriki Super League ya China, huenda akapewa mkataba wa kudumu Old Trafford. (Mail)
Arsenal wameanza mazungumzo kuhusu uhamisho £23m wa kiungo wa kati wa Uturuki wa chini ya miaka 21, Orkun Kokcu, 19. (Mail)
Mshambuliaji wa Everton Muingereza Dominic Calvert-Lewin, 22, yuko kuchezea Toffees kwa muda mrefu kwa kusaini mkataba utakaomalizika 2025. (Times)
Dominic Calvert-LewinHaki miliki ya picha
Everton wanafanya mazungumzo ya kumsajili beki wa Lille Gabriel Magalhaes, 22, ambaye Januari alihusishwa na uhamisho wa kuenda Arsenal na Tottenham. (Independent)
Everton pia wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa Celtic, Odsonne Edouard, 22, baada ya wasaka vipaji wao kufanya ziara kadhaa za kufuatilia mchezo wa kinda huyo wa Ufaransa (Mail)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amepinga tetesi kwamba alijaribu kuwasiliana na Real Madrid katika juhudi za kumsajili kwa kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 23. (Marca)
Dani CeballosHaki miliki ya pichan
Chelsea wanatafakari uwezekano wa kumnunua kipa Mturuki Ugurcan Cakir ,23, wa Trabzonspor - ambaye ananyatiwa na Liverpool - kuchukua nafasi ya kipa wake Mhispania Kepa Arrizabalaga, 25. (Fotospor, via Express)
Winga wa England Jadon Sancho amekataa ofa ya £30,000- kwa wiki ya kujiunga na Manchester City kutoka Borussia Dortmund.(Mail)
Tottenham wako tayari kumpatia mkataba mpya kiungo wa kati wa nyumbani Oliver Skipp, 19. (Football Insider)
Jadon SanchoHaki miliki ya picha
Arsenal wanamfuatilia mshambuliaji wa Gent na Canada Jonathan David, 20. (Goal)
Shirikisho la Soka la Ufaransa limethibitisha kupokea ujumbe wa Paris St-Germain kwamba hawata mshambuliaji wao Kylian Mbappe, 21, kushiriki michezo ya Olimpiki ya majira ya joto nchini Japan. (ESPN)
Arsenal na Everton wamekosa nafasi ya kusaini mshambuliaji wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens, 32, katika msimu wa uhamisho wa wachezaji baada ya kubainika kuwa mkataba wa kumuachilia mchezaji huyo kujiunga na klabu za kigeni ilikamilika Januari 10. (Star)
Kylian Mbappe celebratesHaki miliki ya pichaImage caption
Leicester City wamehusishwa na tetesi za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Marseille Morgan Sanson, 25. (Jeunes Footeux, via Leicester Mercury)

Post a Comment

0 Comments