TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMISI TAREHE 5.3.2020


Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 26, atafikiria kuhamia Manchester United msimu huu. (Goal).Kane hana mpango wa kusaini mkataba mwingine na Tottenham. (Express)
Aresenal wanaweza kufungua njia kwa John Stones, kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu. (90 Min)
Mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig amesema klabu haijapokea ofa yoyote kwa ajili ya mshambuliaji Timo Werner, pamoja na kuwepo kwa nia kutoka kwa Liverpool, Chelsea na Manchester United. (Mirror)

Beki wa kushoto wa Manchester City Angelino, 23, anayeichezea RB Leipzig kwa mkopo, anasema angeondoka City iwapo marufuku ya kucheza michuano ya mabingwa ulaya ingeondolewa. (MEN)
Borussia Dortmund ina uhakika wa kupata saini ya kiungo wa Birmingham City Jude Bellingham,16, msimu huu. (Telegraph)
Birmingham imekana taarifa kuwa imepokea ofa kutoka Dortmund kwa ajili ya Bellingham. (90 Min)
Manchester United bado ina nia ya kumpata Bellingham. (MEN)
Wakati huohuo, Dortmund inaweza kutaka kitika cha pauni milioni 121 kwa ajili ya mshambuliaji Jadon Sancho, 19. (Bild - in German)
Mshambuliaji wa Chelsea Willian, 31, anajiandaa kuukacha mkataba mpya na huenda akahamia Tottenham. (UOL)

Timo WernerHaki miliki ya picha

Chelsea itahitajika kulipa pauni milioni 40 kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Brazil na Porto Alex Telles, 27, kuchukua nafasi ya beki wa kushoto Marcos Alonso,29. (Sun)
Atletico Madrid inamtolea macho kiungo wa Barcelona Ivan Rakitic, 31, msimu huu. (Marca - in Spanish)
Everton, West Ham na Wolves wako kwenye kinyang'anyiro kumsajili winga wa Mexico, Hirving Lozano kutoka Napoli. (Calciomercato - in Italian)
Tottenham imemruhusu kiungo Victor Wanyama, 28, kujiunga na Montreal kwa uhamisho huru. (Standard)
Barcelona itatoa ofa ya mkataba ulio na marekebisho kwa mlinda mlango Marc-Andre ter Stegen. (ESPN)

WanyamaHaki miliki ya pichan

Inter Milan itataka wachezaji watatu kutoka Barcelona kama mabingwa hao wa Uhispania wanataka kumsajili mshambuliaji Lautaro Martinez,22 msimu huu. (Mundo Deportivo, via Mail)
Mlinda mlango wa Schalke Ralf Fahrmann, 31, anayecheza Norwich kwa mkopo, yuko kwenye mazungumzo kuhusu uwezekano wa kujiunga na SK Brann. (Sky Sports)
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anataka klabu kumsajili kuingo wa Olympiacos Mady Camara, 23. (Sdna, via Star)
AC Milan huenda wakamchukua kiungo wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles,22. (Calciomercato - in Italian)

Post a Comment

0 Comments