TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMIS TAREHE 26-03-2020

Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani amedokeza kuwa alijaribu kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 33 pamoja na mshambuliani wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, ambaye alijiunga na AC Milan, dirisha la uhamisho wa wachezaji lilipofunguliwa. (Mail)
Manchester United wanaongoza kinyanganyiro cha kumsaka mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 20, kutoka Borussia Dortmund dirisha la uhamisho litakapofunguliwa tena msimu wa joto. (Independent)
Real Madrid wana matumaini mkataba wa kupata pesa na mchezaji itasaidia kuishawishi Arsenal kumuachilia mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (Star)

Chris SmallinHaki miliki ya picha

Manchester United wako tayari kumruhusu beki wa England Chris Smallin kugeuza mkataba wake wa mkopo Roma kuwa wa kudumu, bora uwawezeshe kumpata beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28. (La Gazzetta dello Sport, via Mail)
Arsenal wamewasilisha ofa ya kumnunua Smalling dirisha la uhamisho litakapofunguliwa msimu wa joto, lakini Manchester United wanataka £25m. (Metro)
Beki wa Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen, 32, amekiri kuwa hana uhakika anataka kusaini mkataba mpya utakamwezesha kusalia Spurs kwa msimu mwingine. (Mirror)

kiungo wa kati wa Real Madrid wa miaka 23-Mhipania Dani CeballosHaki miliki ya picha

Arsenal wanaamini watafanikiwa kuongeza mkataba mwingine wa mkopo na kiungo wa kati wa Real Madrid wa miaka 23-Mhipania Dani Ceballos endapo msimu huu utaendeleazaidi ya Juni 30. (Standard)
Leicester City wamehusishwa na tetesi za uhamisho beki wa Atalanta Ubelgiji Timothy Castagne, 24. (Sport Foot, via Leicester Mercury)
Arsenal huenda wakamnyakua beki Mfaransa Dayot Upamecano kutoka RB Leipzig baada ya kiungo huy wa miaka 21 kuashiria anataka kuhama msimu huu wa joto. (Bild, via Star)
West Brom wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Croatia Filip Krovinovic, 24, kwa mkataba utakaogeuzwa kuwa wa kudumu baada ya mkopo wake kutoka Benfica utapomalizika. (Express and Star)
Waandalizi wa ligi ya soka ya Ulaya wanamatumaini ya kamilisha msimu hu kufikia Juni 30, baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo wiki hii. (Sky Sports)
Chelsea imesitisha mazungumzo ya mkataba wa wachezaji kufuatia janga la coronavirus. Blues wana wachezaji wanne ambao mikataba yao ya sasa inaelekea malizika. Wanne hao ni -Willian, 31, Olivier Giroud, 33, Pedro, 32, na kipa wa Argentina Willy Caballero, 38. (Telegraph)

MessiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Barcelona wanatafakari uwezekano wa kuwapunguzia mshahara wachezaji wao wote kwa asilimia 70 hadi pale amri inayodhibiti matembezi nchini Uhispainia kutokana na janga la corona itakapoondolewa.(Guardian)
Klabu nane za Ligi ya Primia zimeungana kuizuia Manchester City kucheza Champions League msimu ujao kwa kutaka michuano hiyo isitishwe walipowasilisha rufaa dhidi ya marufuku ya miaka miwili waliowekewa na Uefa. (Times,

Post a Comment

0 Comments