mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba Amissi Tambwe , amesema kuwa bado ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, hivyo uongozi wa Yanga umpe dili ili asiani kandarasi mpya.
Tambwe aliwahi kutamba na klabu za Simba na Yanga, amesema anatamani kurudi Yanga kwa sababu ni timu ambayo anaipenda.
Kwa sasa Tambwe hana timu jambo linalompa nafasi ya kujiunga na klabu yoyote ambayo atafika nayo maelewena huku akisisitiza kuwa akipewa nafasi Yanga atatatua tatizo la ukame wa mabao.
“Bado nipo vizuri, sina mzaha nikiwa kwenye lango, Yanga wakinisajili nitawafanyia kazi kweli, unajua mimi nina mapenzi na Klabu ya Yanga, kwa hiyo nikirejea hapo nitaipambania kwa moyo wote,” amesema Tambwe.
Tambwe akiwa Bongo alifunga hattrick nne ambapo alifunga moja akiwa na Simba na tatu akiwa na Yanga zote ilikuwa Uwanja wa Taifa.
0 Comments