TAARIFA MBAYA KWA MASHABIKI WA LIONEL MESSI, NEYMARChama cha soka Amerika Kusini kimetoa taarifa ya kufuta michuano ya Copa America iliyopangwa kufanyika mapema mwaka huu mwezi June. awali michuano hiyo ilipangwa kufanyika nchini Argentina na Colombia  lakini kutokana na kutapakaa kwa virusi vya Corona CONMOBEL wameungana na FIFA pamoja na vyama vingine kama CAF kwa Afrika na UEFA kwa ulaya kuahirisha michuano hiyo.

Ujumbe wa CONMOBEL ulisema " Baada ya taarifa za kichunguzi kuhusiana na COVID-19 na ushauri kutoka mashirika ya Afya duniani, sisi CONMOBEL tunatangaza kuahirisha michuano ya 47 ya COPA AMERICA mpaka mwaka 2021 tarehe 11 June mpaka tarehe 11 julai" Taarifa hiyo iliongeza 

"Shirikisho chini ya raisi wake Alejandro Domínguez pamoja na maraisi 10 wa vyama vya soka chini ya CONMOBEL vimependekeza suala la Afya kuzingatiwa na kuungana na mashirika mengine kukabiliana na janga hili. Afya ni muhimu kwa wachezaji,vyombo vya habari, mashabiki na miji itakayoandaa michuano hiyo"

Kwa wale tuliotegemea kuwaona Lionel Messi na Neymar wakizitetea timu zao kutwaa kombe hilo basi nndoto hizo zimefutika na tunapaswa kusubiri mpaka mwaka 2021


Post a Comment

0 Comments