SVEN : NINAMPELEKA AJIBU NA WENZAKE SIMBA B


Kutokana na kutokuwa na uhakika wa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Ibarahim Ajibu, pamoja na wenzake wasiokuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza, Ijumaa ijayo wanatarajiwa kupelekwa Simba B.
Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amewaandalia wachezaji hao mechi ya kirafiki na Simba B ambayo watacheza kwa ajili ya kuongeza viwango vyao katika kipindi hiki ambacho michuano ya Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa.
Sven alisema kuwa mchezo huo ni moja ya mikakati yake ya kuhakikisha wachezaji wote ambao hawana nafasi katika kikosi chake cha kwanza wanautumia katika kuongeza uwezo wao.
“Licha ya ligi kusimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa, sisi tunaendelea kujifua kama kawaida.
“Tunafanya mazoezi ya nguvu ambayo yanalenga kabisa kuwaweka sawa wachezaji wote ili waweze kuwa fiti na zaidi ni wale ambao hawana nafasi katika kikosi cha kwanza.

Post a Comment

0 Comments