SVEN ATANGAZA KUTUMIA STAILI YA KAMPA KAMPA TENA



Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kikosi chake kiko tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa leo Jumapili kwenye uwanja wa Taifa

Baada ya kuifumua Azam Fc mabao 3-2 Jumatano, Simba iliendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.Sven amesema kuelekea mchezo huo hana mpango wa kufanya mabadiliko yoyote ya uchezaji kwa kikosi chake

Amesema mpaka sasa wamefanikiwa kupitia kandanda lao la pasi fupi fupi na anavutiwa na ushirikiano unaoonyeshwa na wachezaji wake

"Unajua Simba soka hili la pasi imekuwa kama ndiyo utamaduni wake, nimekuwa nikipenda kuona wachezaji wakicheza hivyo kwa sababu inasaidia zaidi timu kutengeza nafasi na ukiangalia tunapambania ubingwa, hatuhitaji kubadili kitu," amesema
Simba imejipanga kuondoka na alama zote tatu hapo kesho huku mashabiki wakija na msemo kuwa Yanga watasema walipataje sare ya mchezo wa kwanza uliopigwa Januari 04

"Kesho ndio watatujua Yanga, tunataka watuambie walipataje sare kwenye mchezo wa kwanza?," kauli ya Mama Simba, Mwanachama na shabiki kindakindaki wa mabingwa hao wa nchi

Post a Comment

0 Comments