mshambuliaji wa KMC Sadala Lipangile amesema kuwa kilichowapa ushindi mbele ya Yanga ni juhudi za wachezaji kujituma ndani ya uwanja bila kuchoka. KMC jana ilishinda bao 1-0 mbele ya Yanga na kuvunja rekodi ya kutoambulia pointi tatu mbele ya Yanga kwenye mechi tatu za Ligi Kuu Bara walipokutana ambapo msimu uliopita wa 2018/19 iliyeyusha pointi zote sita na kwenye mechi ya kwanza msimu huu wa 2019/20 ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1. Lipangile amesema: "Morali kwa sasa kwa wachezaji imerudi na tunatambua kwamba tuna kazi kubwa ya kujinasua hapa kwenye kushuka daraja, ushindani ni mkubwa nasi tutapambana,". Bao la ushindi la KMC lilifungwa na Salim Aiyee dakika ya 62 akiwa ndani ya 18 mabeki wa Yanga walidhani ameotea.
2 Comments
Morali wapi,Yanga walichoka tu na game ya mikia basi
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
Delete