BETI NASI UTAJIRIKE

RIPOTI YA MECHI: YANGA WALIVYOBANWA MBAVU NA NAMUNGO FC



Namungo FC wamelazimisha sare ya 1-1 na vigogo, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Sare hiyo inaifanya Namungo FC iendelee kukamata nafasi ya nne, ikifikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 28, nyuma ya wapinzani wao wa leo, Yanga SC wenye pointi 51 sasa baada ya kucheza mechi 27.


Katika mchezo wa leo, Yanga SC waliocheza bila ya kocha wao Mkuu, Mbelgiji Luc Eymael aliyekuwa anatumkia adhabu ya kazi ambaye alikuwa jukwaani ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao.

Alikuwa ni mshambuliaji wake mpya, Tariq Seif Kiakala aliyefunga kwa kichwa dakika ya sita tu akimalizia krosi ya kiufundi kabisa ya beki wa kulia, Juma Abdul Jaffar Mnyamani.

Namungo FC ikapata pigo dakika ya 23 baada ya mlinzi wake, Carlos Protas kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Hamisi Fakhi aliyekwenda kumalizia vizuri.

Yanga SC ingewa kumaliza kipindi cha kwanza ina mabao hata matatu kama ingeweza kutumia nafasi zake mbili zaidi ilizotengeneza kama si kiungo Mghana, Bernard Morrison na mshambuliaji mzawa, Ditram Nchimbi kukosa mabao ya wazi.

Kipindi cha pili Namungo FC walirejea na mipango mizuri na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kupita kwa mshambuliaji wake Mrundi, Bigirimana Blaise akimalizia pasi nzuri ya kiungo fundi, Lucas Kikoti.

Bao hilo likawapa hali ya kujiamini zaidi Namungo na kuanza kutawala mchezo, kabla ya mabadiliko yaliyofanywa na Yanga kumtoa kiungo Mnyarwanda Patrick Sibomana na kumuingiza mzawa, Mapinduzi Balama kuwarejeshea nguvu wageni.

Kikosi cha Namungo FC kilikuwa; Nourdine Balora, Miza Christom, Jukumu Kibanda, Stephen Duah, Carlos Protas/Hamisi Fakhi dk23, Daniel Joram, Hashimu Manyama, Steve Nzigamasabo, Bigirimana Blaise, Lucas Kikoti na George Makang’a/Abeid Athumani dk54.

Yanga SC; Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohammed, Said Juma ‘Makapu’, Ally Mtoni ‘Sonso’, Papy Kabamba Tshishimbi, Patrick Sibomana/Mapinduzi Balama dk69, Feisal Salum, Ditram Nchimbi/Yikpe Gislain dk89, Tariq Kiakala na Bernard Morrison.  

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, KMC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Alliance FC Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa na Charles Martin Ilamfya yote dakika ya tisa na 80, wakati la Alliance limefungwa na Mnigeria Michael Chinedu dakika ya 90.

Post a Comment

0 Comments