BETI NASI UTAJIRIKE

UEFA WATOA NENO KUHUSU MICHUANO YA EURO 2020 , MAAMUZI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE




Raisi wa shirikisho la soka Ulaya UEFA Bw. Aleksander Ceferin ametangaza rasmi kufuta michuano ya timu za taifa EURO 2020 mpaka mwaka 2021. UEFA wamefikia maamuzi hayo baada ya kufanya kikao kwa nchi wanachama wa shirikisho hilo huku uwepo w COVID-19 ukiwa ni kikwazo kikubwa. 

Nchi za Ulaya zimekumbwa na balaa hilo hatarishi na limezifanya mamlaka mwanachama kuzuia mikusanyiko mbalimbali ikiwemo kusimamisha ligi mbalimbali.  Hata hivyo hali inategemewa kurejea kama awali huku Ligi mbalimbali zikipanga kuendelea kuanzia tarehe 02-04-2020 endapo tu hali itakuwa shwari.

Rais huyo wa UEFA alinukuliwa akisema " Sote tunafahamu janga la virusi hivi lilizua mjadala Ulaya yote kuanzia kwenye soka mpaka maisha ya kawaida. Tunafahamu tunatakiwa kuusimamisha michuano hii ya EURO ili ligi na michuano mbalimbali ya vilabu iweze kumalizika . Hilo halina uhakika kwa sasa lakini tunapaswa kufkiri kuhusu Afya za wachezaji na mashabiki. Lakini pia tunatakiwa tuwaze pia kuhusu Soka kwa ujumla.

"Leo tumeamua kuahirisha michuano ya EURO 2020 na tuna asilimia 100 ya sapoti kutoka nchi wanachama 55,Bodi ya ligi ulaya pamoja na Chama cha vilabu ulaya pamoja na  FIFPRO

Kufutwa kwa michuano ya EURO 2020 kunazipa nafasi ligi mbalimbali kuendelea mara tu janga litakapokwisha lakini pia michuano ya EUROPA na UEFA CHAMPIONS LEAGUE itaendelea kama kawaida.

Post a Comment

0 Comments