BETI NASI UTAJIRIKE

WABRAZIL WA SIMBA KUONDOKA BURE JUNI



Nyota wawili raia wa Brazil Tyrone Da Silva na Gerson Fraga wako ukingoni mwa mikataba yao waliyosaini mwaka jana.Nyota hao kila mmoja alisaini mkataba wa mwaka mmoja na mpaka kufikia mwezi Juni watakuwa wachezaji huru

Tayari tetesi zimezagaa kuwa hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao kwani hawatapewa mikataba mipya.Ukifanya tathmini ya kawaida kabisa utaweza kukubali kuwa Fraga ameonyesha kiwango cha kuridhisha katika mechi nyingi alizopata nafasi
Anaweza asiwe mchezaji bora sana lakini ana vitu vingi vinavyoweza kuisaidia timu pale inapokuwa imekwama

Rejea magoli yake mawili kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union
Ni mchezaji mwenye juhudi, jasiri na anaweza kucheza soka la aina zote, kistaarabu au kibabe

Kwa Fraga pengine Simba itahitaji kupitia uamuzi wake mara mbili kabla ya kuamua kumnyima mkataba.Upande wa Tairone, nadhani hataongezewa mkataba, hilo liko wazi. Ni mchezaji mzuri lakini nadhani Simba inahitaji ubora zaidi yake

Nyota mwingine Wilker Da Silva aliondoka mapema tu mwezi January
Nadhani huyu alipata bahati tu ya kusajiliwa Simba, lakini hakuwa mchezaji mwenye maajabu

Post a Comment

0 Comments