Nyota wa Yanga ambaye kwa sasa ameiteka mioyo ya mashabiki, Bernard Morrison, amesema anafurahi kuona 'amekubalika' mapema ndani ya klabu hiyo na hali hiyo inampa nguvu ya kujipanga kufanya makubwa zaidi
Wiki iliyopita Morrison alisaini mkataba mpya ambao utamuweka Jangwani kwa miaka miwili. Awali Morrison alikuwa akiwindwa na klabu ya Simba
Morrison amesema ataongoza mapambano kuhakikisha wanashinda mechi zao za ligi zilizobakia na mashindano ya Kombe la FA.
Aidha, Mshambuliaji huyo amesema kuwa 'mapenzi' wanayopata wachezaji wa timu hiyo kutoka kwa mashabiki wa Yanga ni sababu inayowafanya wajitume katika kila mechi wanayocheza na kusahau changamoto zinazowakabili.
"Ningependa kuwashukuru mashabiki kwa kunikubali, nimekuwa na wakati mzuri, nimekuwa nikipata zawadi mbalimbali kutokana na uchezaji wangu, hii inanifanya nijipange zaidi kuisaidia timu yangu, nimejifunza vitu vingi nilipokuwa Orlando Pirates," amesema Morrison.
"Ninaheshimu ajira yangu ndani ya Yanga, nitaitumikia kwa nidhamu, mipango yangu ni kutimiza malengo yangu, lakini huu ni mpira, kwa sasa nitaelekeza nguvu na akili zangu Yanga"
0 Comments