NDANDA FC YAPIGWA FAINI YA MILIONI 1 KISA CHAELEZWA


Ndanda FC imetozwa faini ya Tsh 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la timu hiyo kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi na kuliacha gari tupu likipita katika mlango rasmi katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar Februari 29, 2020 uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.
Adhabu inatolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 14(43) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Post a Comment

0 Comments