MTIBWA SUGAR WAPO TAYARI KUWAVAA COSTAL UNIONMtibwa Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu Zuber Katwila ina mtihani mwingine kesho mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani.

Mchezo wao uliopita waiwa Uwanja wa nyumbani, Gairo walikubali sare ya kufungana bao 1-1 na Biashara United.
Katwila amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya kutokana na ushindani uliopo ndani ya ligi.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14  ina pointi 33 kibindoni baada ya kucheza mechi 29 kwenye Ligi Kuu Bara.

Coastal Union ipo ndani ya tano bora ikiwa nafasi ya tano ina pointi 46 imecheza mechi 28.

Post a Comment

0 Comments