Mshambuliaji wa Yanga, Ditram Nchimbi, amesema anataka kuanzia benchi kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji huyo aliyetua Yanga usajili wa dirisha dogo akitokea klabu ya Polisi Tanzania, amesema mara nyingi amefanya vizuri akitokea benchi kwani huwa anakuwa tayari ameusoma mchezo
"Kwangu huwa naona nafanya vizuri ninapotokea benchi na kwenda kubadili mchezo, ninapokuwa nje mara nyingi nausoma mchezo na nikiingia ninakuwa na jukumu la kufanya timu yangu iwe bora zaidi," amesema Nchimbi
"Siwapangii benchi la ufundi kikosi au namna ya kunitumia lakini kwa sababu wote tunahitaji matokeo ya ushindi katika mechi na Simba lakini nikianzia benchi nina uhakika nitafanya mambo makubwa nikiingia"
Nchimbi ameifungia Yanga mabao mawili na pia akitoa pasi mbili za mabao. Mafanikio hayo aliyapata katika mechi zote ambazo alianzia benchi
Haitashangaza kama kocha Luc Eymael atamtumia kama super-sub kwenye mchezo huo ambao utaanza saa 11 jioni.Mcongoman David Molinga ambaye alikosa mchezo wa duru ya kwanza huenda akaanza kwenye mchezo huo sambamba na Tariq Seif Kiakala
0 Comments