Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema kuwa anausubiri kwa hamu mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, March 08 2020.Nchimbi amekuwa kwenye kiwango bora siku za hivi karibuni ambapo kwenye mchezo dhidi ya Alliance Fc alifunga mabao yote mawili ya Yanga waliposhinda 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa
Mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa amesema mchezo wa watani wa jadi ni mchezo wa heshima hivyo kama atapewa nafasi ya kocha Luc Eymael, atahakikisha anaacha alama
"Mchezo dhidi ya Simba ni mchezo mgumu usiotabirika kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hizi. Kwetu sisi wachezaji ni mchezo ambao unaweza kukupaisha au kukushusha chini kama hutafanya vizuri. Mimi binafsi nimejipanga kuhakikisha nafanya vizuri kama kocha atanipa nafasi," amesema Nchimbi
"Hatukupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza lakini tumejipanga kufanya vizuri kwenye mchezo wa Jumapili. Muhimu ni kwa mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi watuunge mkono ili tuweze kutimiza malengo tuliyojiwekea"
Nchimbi alicheza mchezo wa kwanza uliopigwa Januari 04 2020 lakini wakati ulendio kwanza alikuwa amejiunga na timu akitokea klabu ya Polisi Tanzania
Kwa sasa ni mchezaji tofauti akiwa miongoni mwa wachezaji wanaoaminiwa na kocha Luc Eymael
0 Comments