KAGERE ATOBOA SIRI YA MAFANIKIO YAKE SIMBA



Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere ametaja siri ya mafanikio yake ni kujituma, kushirikiana vizuri na wenzake na kuhakikisha kila siku anakuwa bora kwa kufanya mazoezi
Msimu uliopita,

Kagere aliibuka mfungaji bora wa VPL baada ya kufunga mabao 23
Tayari msimu huu amefunga mabao 19 na ni wazi anaelekea kuwa mfungaji bora kwa msimu wa pili mfululizo

Nyota huyo raia wa Rwanda amesema anachofanya kila siku ni kuhakikisha anakuwa bora kuliko wachezaji wazawa kwani anaamini dhumuni la yeye kusajiliwa na Simba ni pamoja na kuonyesha kuwa ana kitu zaidi ya wachezaji wa ndani

"Ukiwa mchezaji wa kigeni lazima uonyeshe utofauti na wachezaji wa ndani. Hivyo mimi huwa najituma zaidi ili kuhakikisha nakuwa bora wakati wote. Jambo moja kubwa huwa nahakikisha sipati majeraha ya mara kwa mara na nakuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga kila msimu," amesema Kagere

Kagere kwa sasa yuko kwao Rwanda na familia yake wakati huu mapumziko ya kudhibiti maambukizo ya virusi vya Corona

Post a Comment

0 Comments