Mshambuliaji wa Namungo Fc Reliants Lusajo ni miongoni mwa nyota wanaotajwa kuwa wanaweza kusajiliwa na Yanga mwezi Juni dirisha la usajili litakapofunguliwa
Nyota huyo yuko ukingoni mwa mkataba wake na Namungo ambao unamalizika mwishoni mwa msimu
Inaelezwa Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael amevutiwa na uwezo wa mfumania nyavu huyo ambaye ameifungia Namungo mabao 11 kwenye ligi mpaka sasa
Mwenyewe ameeleza kuzisikia tetesi za kutakiwa na Yanga lakini amesema wakati ukifika itafahamika
"Mkataba wangu umebaki miezi mitatu, hivyo naruhusiwa kufanya mazungumzo na timu yoyote. Taarifa za mimi kuhusishwa Yanga nimezisikia lakini siwezi kusema chochote kwani huu sio wakati wake"
"Wakati ukifika kila kitu kitawekwa hadharani," alisema Lusajo
Eymael tayari amepewa ruhusa ya kuanza kukijenga kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao ambapo kwa sasa Yanga imeanza na mchakato wa kuhuisha mikataba ya wachezaji ambayo iko ukingoni
0 Comments