GADIEL MICHAEL AJIPANGA KUJA KIVINGINEMlinzi wa kushoto wa Simba Gadiel Michael anajifua kujiweka sawa baada ya wachezaji kupewa mapumziko ya siku saba kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona

Nyota huyo aliyetua kwa mabingwa hao wa nchi akitokea klabu ya Yanga, amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi mbele ya nahodha msaidizi Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr'
Tangu ujio wa kocha Sven Vandenbroeck, Gadiel amekuwa na nafasi finyu kwenye kikosi cha kwanza hivyo kulazimika kufanya kazi ya ziada kurejea kikosini

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha misimu mitatu, Gadiel hakuitwa timu ya Taifa kwa ajili ya michuao ya CHAN

"Timu yetu ina ushindani mkubwa wa namba. Nitaendelea kujituma ili kuhakikisha nikipewa nafasi simuangushi Mwalimu," amesema Gadiel

Post a Comment

0 Comments