BETI NASI UTAJIRIKE

SHIKHALO ALIPIGIA HESABU KOMBE LA FA



Mlinda lango wa Yanga farouq Shikhalo amekiri kwa sasa sio rahisi wao kutwaa taji la Ligi Kuu kutokana na changamoto walizokutana nazo.Hata hivyo anaamini wakiwa imara wana nafasi ya kushinda taji la FA

Shikhalo anayechuana vikali na Metacha Mnata kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, amesema kwa jitihada wanazofanya, wanastahili kumaliza msimu wakiwa angalau na taji moja

"Kwa sasa ni wazi nafasi yetu ya kutwaa ubingwa ni finyu sana. Kuna makosa mengi tulifanya kwenye hesabu zetu huko nyuma, lakini mimi naamini tukiweka juhudi zaidi, tunaweza kushinda FA"
"Kila mmoja anataka tupate nafasi kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao, nadhani tuna kila sababu ya kupambana kuhakikisha tunashinda taji hilo," alisema Shikhalo

Shikhalo alitua Yanga mwanzoni usajili wa msimu huu akitokea klabu ya Bandari Fc ya Kenya

Post a Comment

0 Comments