KAKOLANYA BADO YUPO SANA SIMBAMlinda lango wa Simba, Beno Kakolanya, amesema ataendelea kukitumikia kikosi hicho, licha ya kukosa namba ya kudumu kutokana na ushindani.Kauli hiyo ni kama salamu kwa mpinzani wake Aishi Manula kuwa asibweteke akifahamu mwenzake huyo yupo katika hesabu kali jinsi ya kupata nafasi Msimbazi na si kutimka.

Kakolanya amekuwa akitumika kama kipa namba mbili katika kikosi cha Simba, nyuma ya Manula.
Kakolanya aliyetua Simba baada ya kuvunja mkataba wake na Yanga, amesema bado ana nafasi kubwa ya kuitumikia timu yake, licha ya ushindani anaoupata kutoka kwa Manula.

"Ni kawaida kwa kocha kumpa nafasi mchezaji anayemuona yupo vizuri, silaumu Manula kupangwa, naamini hata mimi nina nafasi, siku yangu haijafika, kama ikifika hakuna kitakachozuia," Kakolanya amenukuliwa

"Binafsi naumia kuona nimeisaidia timu yangu michezo michache katika ligi, lakini bado ipo mingine niliyokaa langoni kama mechi za Mapinduzi, pamoja na FA, hivyo inawezekana Manula akatumika katika ligi na mimi nikapata nafasi kwenye mashindano mengine, kikubwa wote tunaisaidia Simba ishinde tu"

Kipa huyo amedaka michezo saba ya Ligi Kuu Bara kati ya 28, ambayo Simba imecheza.
Kwa sasa Simba inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 71, baada ya kucheza michezo 28, sawa na Azam wanaoshika nafasi ya pili kwa pointi 54.

Post a Comment

0 Comments