BETI NASI UTAJIRIKE

REKODI YA AISHI MANULA LIGI KUU YAWATISHA WAPINZANI WAO YANGA


Mlinda lango namba moja wa Simba, Aishi Manula, ameendelea kuwafunika makipa wengine Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushindwa kufikia rekodi yake.
Manula aliyedaka michezo 18,  akiwa na kikosi chake cha Simba msimu huu,  ameruhusu mabao sita
Anayemfuatia ni kipa wa Azam Razack Abalora ambaye amefungwa mabao saba baada ya kukaa langoni mara 13
Kwa upande wa kipa wa timu ya Yanga, Faruk Shikalo,  ameruhusu mabao 12, baada ya kukaa langoni mara 13, wakati kipa wa Kagera Sugar Benedict Tinocco ameruhusu mabao 14  akidaka michezo 16.
Manula amekuwa ni kipa bora katika misimu minne mfululizo akifukuzia kutwaa tuzo nyingine msimu huu,  unaoelekea ukingoni
Baada ya kuachwa nje kwa zaidi ya mwezi mmoja kufuatia kuboronga mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga, Manula amesahihisha makosa yake na sasa ameonekana kuimarika zaidi

Post a Comment

0 Comments