BETI NASI UTAJIRIKE

MIKEL ARTETA NA HUDSON ODOI WAPATWA NA JANGA LA CORONA



Kocha mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta na kiungo wa timu ya Chelsea, Callum Hudson-Odoi wote wamegundulika na Virusi vya Corona baada ya kufanya vipimo.

Arteta mwenye miaka 37 amekuwa mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa amekumbwa na Corona ndani ya Ligi Kuu England baada ya mlipuko wa ugonjwa huo ulioanza kuenea kwa kasi tangu mwezi Januari.

Kwa sasa yeye na wafanyakazi wenzake ndani ya Arsenal watawekwa kwenye uangalizi maalumu ikiwa ni agizo la Serikali ili kupewa matibabu na kuepusha kusambaza kwa wengine.

Pia Klabu ya Chelsea imethibitisha kuwa Hudson-Odoi mwenye miaka 19 amekutwa na Corona jambo hilo limewafanya wafunge kambi yao ya mazoezi iliyokuwa Cobham huku wafanyakazi waliokuwa karibu na nyota huyo wakipewa uangalizi maalumu.

Arsenal Ilikuwa inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Brighton Jumamosi mechi hiyo imeahirishwa na imeelezwa kuwa kutakuwa na mkutano wa dharula ili kujadili kuhusu kusimamisha Ligi Kuu ya England kutokana na Corona.

Post a Comment

0 Comments