Shabiki na MC maarufu wa klabu ya Yanga mkoani Iringa Bw.Justin Muhanila amewataka mashabiki wa soka nchini kuchukua tahadhari kukabiliana na changamoto za ugonjwa wa Corona na kufuata maelekezo yatolewayo na wataalamu wa afya
Mc Muhanila Justin amenukuliwa akisema "ni vyema tukafuata taratibu zilizowekwa na serikali ili kukabiliana na janga hili la kidunia, watanzania tuache ubishi na tufuate maelekezo ya wataalamu wa kiafya. Tumeshuhudia nchi za Asia na Ulaya zikiathirika sana mbali na wao kuwa na teknolojia lakini wameshindwa kuudhibiti ugonjwa huu je janga hili likija kwetu si itakuwa hatari zaidi." Bw.Justin aliendelea kwa kusema "
"Haijalishi wewe upo Yanga ama Simba ni muhimu kuepuka kukaa kwenye misongamano,kukumbuka kunawa mikono lakini pia uhisipo dalili zozote ufike hospitali kwa vipimo"
alipoulizwa kuhusu maendeleo ya Yanga na changamoto mpya za mdhamini wa klabu hiyo alisema
" Suala la Yanga linahitaji ufafanuzi yakinifu ila kwa sasa tupambane na janga hili la kidunia"
0 Comments