Ridhiwani ametoa maoni yake kufuatia tukio la Clatous Chama wa Simba kumkanyaga kwa makusudi kiungo wa Yanga Feisal Salum kwenye mchezo wa watani wa jadi uliopigwa juzi kwenye uwanja wa Taifa ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Ameitaka TFF ichukue hatua bila ya kusubiri malalamiko kutoka kwa klabu ya Yanga
Ikumbukwe tukio kama hilo lilifanywa na beki wa Simba Paschal Wawa dhidi ya Ditram Nchimbi kwenye mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
Hata hivyo TFF haikumchukulia hatua yoyote Wawa licha ya kuonekana dhahiri akimkayaga Nchimbi kwa makusudi
"Na hili nalo TFF mnataka Yanga waje kulalamika? Lindeni Wachezaji wa timu ya taifa. Ninyi ndiyo wasimamizi wa mpira Tanzania. Tendeni haki kama kauli mbiu inavyosema ' Our Game Is Fairplay', Be fair," aliandika Ridhiwani kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.Jana Chama aliomba radhi kwa tukio hilo lisilo la kiungwana alilomfanyia Fei Toto
Wadau wamempongeza Chama kwa kuwa muungwana lakini bado TFF ina nafasi yake ya kuchukua hatua ili kuhakikisha matukio haya hayaendelei kujitokeza
0 Comments