BETI NASI UTAJIRIKE

MASHINE NNE KUTUA YANGA DIRISHA KUBWA



Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kuwa timu hiyo itasajili nyota wanne wa kigeni yakiwa ni mapendekezo ya kocha Luc Eymael

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbulia amesema Eymael amewasilisha ripoti ya maboresho ya kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao

"Mwalimu ametuachia ripoti yake ya usajili ambayo tayari wadhamini wetu kampuni ya GSM wameanza kuifanyia kazi," amesema Bumbuli

"Mwalimu amehitaji wachezaji wanne wa kigeni ambao ni beki, kiungo, winga na mshambuliaji"

"Pia amependekeza wachezaji ambao mikataba yao imemalizika lakini anahitaji kuwa nao msimu ujao"

"Tunaendelea na mazungumzo na wachezaji nane ambao mikataba yao iko ukiongoni"

Post a Comment

0 Comments