MORRISON ANUSURIKA RUNGU LA TFF MECHI NA SIMBA


Mashabiki wa Yanga hawapaswi kuwa na hofu ya kumkosa mshambuliaji wao Bernard Morrison kwenye mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili ijayo kwa kuwa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inatarajiwa kukutana wiki ijayo

Morrison pamoja na kiungo wa Simba Jonas Mkude wanatarajiwa kujadiliwa na Kamati hiyo kufuatia matukio ya utovu wa nidhamu waliyofanya katika mechi zilizopita
Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu Wakili, Kiomoni Kibamba, amesema ilikuwa wakutane Jumapili iliyopita, lakini walishindwa kutokana na ratiba za wajumbe kutokuwa rafiki kuwawezesha kukutana.

"Ili kamati isikilize kesi, lazima idadi itimie au kuwa nusu yake, lakini kutokana na majukumu mbalimbali kamati haikuweza kukutana.

"Mwisho wa wiki hii, wajumbe wengi wa kamati ya nidhamu tutakuwa Dar es Salaam, hivyo tutakutana na kupitia kesi zote zilizoletwa mezani, bila shaka hadi itakapofika Jumatatu ijayo, masuala yote tutayamaliza."

Uwepo wa Morrison kwenye mchezo wa Jumapili ni habari njema kwa Yanga kwani nyota huyo raia wa Ghana amekuwa na mwanzo mzuri kunako klabu hiyo
Tangu awasili mwezi Januari, Morrison ameifungia Yanga mabao matatu na kutoa pasi tano za mabao.Hizo ni takwimu za juu sana ukilinganisha na muda ambao amekaa Yanga

Post a Comment

0 Comments