MANULA: MORRISON ANASTAHILI PONGEZI KWA BAO ALILONIFUNGAMlinda lango wa Simba Aishi Manula amesema bao alilofungwa na Bernard Morrison kwenye mchezo wa watani wa jadi lilikuwa la viwango vya hali ya juu hivyo hapaswi kulaumiwa

Akohojiwa na redio moja maarufu mapema leo, Manula alisema mpira ule wa adhabu ulipigwa kwa ufundi wa hali ya juu na Morrison anastahili pongezi

"Sidhani kama nastahili kulaumiwa kwakufungwa bao lile, pengine mpigaji Bernard Morrison ndiye anayestahili kupongezwa," alisema

"Ulikuwa ni mpira mgumu kwa kipa yeyote kuweza kuufikia.."

Morrison alifunga bao hilo kwenye dakika ya 44 na kuihakikishia Yanga ushindi muhimu dhidi ya watani zao

Lilikuwa bao lililotokana na mpira wa adhabu nje kidogo ya 18 ambao ulitokana na kiungo wa Simba Jonas Mkude kumfanyia madhambi Morrison mwenyewe

Post a Comment

0 Comments