BETI NASI UTAJIRIKE

MWAKALEBELA AFUNGUKA MBIO ZA UBINGWA


Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema bado timu yake iko kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu.Yanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 50, imezidiwa na Simba alama 18
Hata hivyo Yanga ina michezo miwili kibindoni ambayo kama watashinda yote watapunguza tofauti ya pointi hizo na kuwa 12

Mwakalebelela amesema Yanga bado ina michezo 13 wakati Simba wana michezo 11 hivyo hawawezi kusema mbio za ubingwa zimemalizika

"Bado mechi zipo nyingi, tunachopaswa kufanya ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michezo yetu yote iliyobaki. Kwanye mpira wa miguu jambo lolote linaweza kutokea hivyo hatupaswi kukata tamaa," amesema Mwakalebela

Kesho Alhamisi Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kumenyana na KMC kisha kuelekea Ruangwa mkoani Lindi kuwakabili Namungo Fc ukiwa ni mchezo wa kwanza baina ya timu hizo msimu huu ambao utapigwa March 15
Yanga pia bado haijacheza na Mwadui FC msimu huu

Post a Comment

0 Comments