BETI NASI UTAJIRIKE

LIONEL MESSI AUNGANA NA CRISTIANO RONALDO KUPAMBANA NA CORONA



Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi ameungana na Cristiano Ronaldo kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona. Lionel Messi ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wachukue tahadhali ili kuukabili ugonjwa huo uliotapakaa dunia nzima.

Ligi kuu Hispania ni moja ya ligi zilizosimama kwa wiki mbili ili kukabiliana na janga hilo huku Barcelona wakiwa juu ya Real Madrid kwa pointi 2 zaidi. Lionel Messi amewataka wachezaji wenzake kutulia majumbani mwao kipindi hiki kukiwa na taharuki klabui hapo kwa mchezaji mmoja wa Barcelona Basket Ball kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Lionel Messi anaungana na Ronaldo ,Pogba ,Klopp na wachezaji wengine kufikisha ujumbe wa kujikinga kwa mashabiki wa soka duniani kote.Lionel Messi alinukuliwa akisema 

"Hizi ni siku hatarishi kwa kila mmoja wetu, kila mtu anaogopa kwa kila kinachotokea na tunataka kusaidia kwa kuwakaribu na waathirika au waliopoteza ndugu zao au hata wale wanaotoa misaada mahospitalini . Ninataka niwape moyo wale wote waliofikwa na majanga"

Lionel Messi amefunga mabao 19 kwenye michezo 22 aliyocheza msimu huu na bao lake la mwisho kabla  ligi haijasimama ni dhidi ya Real Sociedad mchezo uliopigwa  machi 7 Nou Camp.

Lionel Messi alisisitiza kwa kusema " Afya ni kitu cha muhimu zaidi , ni wjibu wetu kufuata maelezo ya mashirika ya afya  na mamlaka za kijamii, Na hiyo ndiyo njia sahihi ya kujikinga "

Post a Comment

0 Comments