LIONEL MESSI AIRUDISHA BARCELONA KILELENI LA LIGA


Mshambuliaji hatari wa Barcelona ameendele kuwa mkombozi wa klabu hiyo yenye maskni yake Camp Nou baada ya kufunga bao muhimu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Real Sociedad

Dakika ya 81 Barcelona walipata penati iliyopigwa na Lionel Messi na kupelekea wao kuibuka na ushindi wa bao moja wakipata pointi 58 kwenye michezo 28 waliyocheza msimu huu.nafasi ya pili ni Rel Madrid yenye pointi 56 wakiwa na mchezo siku ya leo dhidi ya Real Betis

Ushindi huo umekuja baada ya siku 6 zilizopita kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao Real Madrid. Goli la Lionel Messi linamfanya kuongoza  orodha ya wafungaji bora La Liga akiwa na magoli 19 akimuach mbali Kareem Benzema wa Real Madrid mwenye magoli 13 msimu huu. 

Haya ni Matokeo mengine ya La Liga 


Post a Comment

0 Comments