Licha ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kutangaza kusitishwa kwa mechi za kuwania kufuzu kwa michuano ya AFCON 2021 ambazo zilikuwa zipigwe mwishoni mwa mwezi huu, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema kambi ya kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kwa wachezaji wa ndani haitavunjwa
Jana TFF ilithibitisha kupokea barua kutoka CAF ambayo inaeleza kusitishwa kwa mechi hizo kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona huku hatma ya michuano ya CHAN ikisubiri uamuzi wa mwisho
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ugonjwa huo kuwa janga la dunia. tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) limewashauri wanachama wake kusitisha michuano yote ya Kimataifa iliyopaswa kufanyika mwezi huu na April kutoka na janga la Corona
Karia amesema Stars itaendelea na kambi yake hasa kwa ajili ya wachezaji wa ndani ili wawe tayari kwa mabadiliko yoyote ambayo yanaweza kutokea
"Kambi ya timu ya Taifa itaendelea kama kawaida kwa ajili ya wachezaji wa ndani kupata nafasi ya kuendelea kujiandaa kwa lolote litakalo amuliwa licha ya Barua ya CAF kueleza kwamba, mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani yatatolewa maamuzi baada ya kamati maalumu iliyotumwa Cameroon kuleta majibu kuhusu usalama kuhusiana na Corona," amesema Karia
0 Comments