Licha ya kuwa ya mwisho mwenye msimamo wa ligi timu ya Singida United imepanga kuishangaza Simba kwa kuifunga katika mchezo wa ligi utakaopigwa uwanja wa Uhuru leo saa 10 jioni.
Simba itakuwa inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kukubali kipigo cha bao moja kutoka kwa watani wao Yanga siku ya Jumapili.Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Festo Sanga amesema kikosi chao kipo kamili na wana uhakika wa kupata matokeo ya ushindi mbele vinara hao wa ligi.
Sanga amesema katika mchezo wa leo hawatakuwa na kocha wao mkuu Ramadhani Nsanzurwimo ambaye hakusafiri na timu kutokana na kuugua.
"Kikosi kipo kamili na tuna uhakika wa kupata ushindi wa pointi tatu dhidi ya Simba. Tunataka ushindi tutakao upata tumpe pole kocha wetu ambaye anaumwa," alisema Sanga.
Kuhusu kuwa kwenye nafasi ya kushuka daraja kutokana na kuburuza mkia wakiwa na alama 12 pekee Sanga amesema hawawezi kushuka na wataanza kukusanya alama tatu leo kutoka kwa Simba
Wakati Sanga akitoa tambo hizo, Simba imepania kwelikweli kuifumua Singida United ili kupoza machungu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga
0 Comments