Baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Machi Mosi, KMC imemaliza hasira zake kuwa kushinda mechi nne mfululizo ndani ya mwezi Machi.
Mabao ya KMC ilipocheza na Simba yalifungwa na kiungo Luis Miqussone jambo lililowaongezea hasira KMC ambayo inahaha kujinasua kushuka daraja kwenye msimamo ipo nafasi ya 15 na ina pointi 33 baada ya kucheza mechi 29.
Mechi nne ilizocheza KMC sawa na dakika 360 imefunga mabao matano na kufungwa bao moja huku ikivuna pointi 12 na kupoteza pointi tatu kati ya 18 ilizokuwa ikizisaka mwezi Machi.
Matokeo hayo ilikuwa hivi:- KMC 1-0 JKT Tanzania, Machi 5, KMC 2-0 Mbao Machi 7, KMC 1-0 Yanga,Machi 12, KMC 2-1 Alliance, Machi 15.
Mshambuliaji wa KMC, Charlse Ilanfya aliliambia championi Jumatano kuwa kwa sasa kazi ndo inaanza kwani wanapambana ili kubaki ndani ya ligi.
0 Comments