KOCHA WA NAMUNGO FC AMZUNGUMZIA MEDDIE KAGERE " TERMINATOR"


Kocha Mkuu wa Namungo FC Hitimana amesema kuwa kwa kasi wanayokwenda nayo Simba ndani ya Ligi Kuu Bara ni nafasi ya mshambuliaji wao Meddie Kagere kufunga mabao mengi na kuvunja rekodi yake ya msimu uliopita.
Kagere msimu wa 2018/19 alifunga mabao 23 kwenye ligi na kwa sasa msimu wa 2019/20 ametupia mabao 19 timu yake ikiwa imebakiwa na mechi kumi mkononi kumaliza ligi.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja ili kupambana na kusambaa kwa virusi vya Corona ambapo Serikali imezuia mikusanyiko isiyo ya lazima.

  Thiery ambaye alicheza na Simba kwenye mchezo wa Ligi  
Kuu Bara na kukubali kichapo 
cha mabao 3-2 Uwanja wa Taifa amesema kuwa kasi ya Kagere haizuiliki.
Kagere ni mshambuliaji halisi ambaye anategemea kutengenezewa na kumalizia kwa kuwa wachezaji wenzake wameshamtambua na anafunga akipata nafasi naona kabisa anavunja rekodi yake ya msimu uliopita na atafunga mabao mengi zaidi ya 23.
“Nimecheza na Yanga pamoja na Simba zote ni timu nzuri na zina wachezaji wazuri lakini kwa sasa naona mbio za kiatu zitaongezewa kasi na yeye mwenyewe, timu inacheza ikiwa haina presha ya kupoteza jambo hilo linawapa nafasi ya kucheza vile wanavyotaka na kuwapa uhuru wa kufunga,” amesema.

Post a Comment

0 Comments