KOCHA WA NAMUNGO ATAJA KINACHOWAPA KIBURI LIGI KUUKocha Mkuu wa Namungo Hitimana Thiery  amesema kuwa timu yake inapambana kwa hali na mali kupata matokeo chanya bila upendeleo wowote.

Thiery amekiongoza kikosi chake kwenye mechi 27 kipo nafasi ya nne kikiwa na pointi 49 kibindoni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakionyesha juhudi kwenye mechi zote wanazocheza jambo linalowapa matokeo licha ya kupitia kwenye ratiba ngumu ya kusafiri.

"Tumekuwa tukipata matokeo mazuri wakati mwingine mabaya lakini yote yanatokana na juhudi za wachezaji wangu sipendelewi wala sibebwi na yeyote yule, sapoti ya mashabiki ni kubwa na tunabanwa na ratiba hasa kusafiri kunaleta uchovu kwa wachezaji,'" amesema.

Post a Comment

0 Comments