BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA NAMUNGO ATAJA SABABU ZINAZOWAPA MATOKEO UWANJA WA MAJALIWA



Kocha Mkuu wa Namungo FC Hitimana Thiery  amesema kuwa sababu kubwa inayowafanya wapete wakiwa Uwanja wa Majaliwa ni sapoti ya mashabiki.

Namungo kwenye mechi 14 za Ligi Kuu Bara alizocheza Uwanja wake wa nyumbani  amepoteza mechi moja mbele ya Coastal Union amelazimisha sare nne na kusepa na ushindi mechi tisa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wamekuwa wakipata nguvu kubwa kutoka kwa mashabiki wanaoipa sapoti timu yao jambo linalowaongezea nguvu.

"Tunakuwa nyumbani na tunafanya kazi ambayo ni ngumu kuwapa furaha mashabiki, hakuna namna nyingine ambayo tunaitumia zaidi ya sapoti ya mashabiki na wachezaji kujiamini," amesema.

Sare ya kufungana bao 1-1 na Yanga inawafanya Namungo wawe ndani ya tano bora wakiwa nafasi ya nne kibindoni pointi 50 baada ya kucheza mechi 28. 

Post a Comment

0 Comments