KOCHA MTIBWA ATOA SABABU ZA WAO KUFANYA VIBAYA LIGI KUU


Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Zuberi Katwila amesema kuwa vijana wake wanakosa utulivu wanapoingia kwenye 18 jambo linalowapa wakati mgumu wa kupata matokeo.

Mtibwa Sugar, jana Machi 14 ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Biashara United kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Gairo, Morogoro.

Biashara United walianza kupachika bao la kuongoza dk ya 45+2 kupitia kwa Ramadhan Chombo na liliwekwa sawa na Mtibwa Sugar dk ya 79 kupitia kwa Jaffary Kibaya na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

"Kushindwa kupata matokeo nyumbani inaumiza na kikubwa ni vijana wangu wanashindwa kuwa watulivu wanapoingia ndani ya 18 jambo hili linafanya tupate tabu kutafuta matokeo," amesema.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 33 imecheza mechi 29 huku Biashara United ikiwa nafasi ya 10 ina pointi 40 na imecheza mechi 29.

Post a Comment

0 Comments