Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa klabu ya Simba kwenye mchezo ambao utapigwa leo Jumapili katika uwanja wa Taifa
Hata hivyo amesema kikosi chake kimejiandaa kikamilifu akiwaalika mashabiki kujitokeza dimbani hapo kushudia burudani
"Tunafahamu tunakwenda kucheza na timu nzuri, timu ambayo wachezaji wake wamekuwa pamoja kwa miaka miwili au zaidi. Tumefanya maandalizi ya kutosha kuweza kufanya vizuri kwenye mchezo huo," amesema'
"Mashabiki watarajie kupata burudani nzuri kutoka kwetu. Wale waliotizamana mchezo wa el-classico kati ya Real Madrid dhidi ya Fc Barcelona ambao ulipigwa hivi karibuni, watarajie burudani kama ile kwenye mchezo wa kesho"
Nae nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amesema wamejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huo.Beki huyo mahiri wa kulia amesema wanafahamu wanachohitaji mashabiki wao ni furaha hivyo watapambana kuhakikisha wanaibuka washindi baada ya dakika tisini
"Sisi tuko tayari kwa mchezo, tumejiandaa kiakili na kimwili kuwapa furaha mashabiki wetu. Tunawaomba waje kwa wingi kesho, tunawaahidi watafurahi baada ya dakika tisini," amesema
0 Comments